Home Uncategorized SABABU YA SAIDO KUWA NA TIMU MKOANI YATAJWA

SABABU YA SAIDO KUWA NA TIMU MKOANI YATAJWA


 KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze, amesema amemuagiza kiungo mpya wa timu hiyo, Said Ntibazonkiza ‘Saido’ kuangalia kwa umakini namna viwanja vya mikoani vilivyo na kumtaka kuja na mbinu ambayo itaisaidia timu katika mechi za nje ya Dar.

 

Kaze amesema sababu kubwa ya kusafiri na kiungo huyo kwenda Shinyanga ni kwa kuwa anataka ayazoee mazingira hayo mapema kabla hajaanza kuitumikia klabu hiyo, lakini kubwa zaidi atumie uzoefu wake wa kucheza soka nje na ndani ya Afrika kuja na mbinu itakayoisadia Yanga kupata matokeo mazuri kwenye viwanja visivyo na ubora mzuri.


Yanga ambayo Desemba 12 ilicheza na Mwadui kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, ilisafiri na nyota wake huyo ambaye ilimsajili hivi karibuni, lakini bado hajaanza kuitumikia hadi usajili wa dirisha dogo utakapofunguliwa Desemba 15, mwaka huu.


Niliamua kusafiri na Said kwa sababu nilitaka ayafahamu mazingira ya viwanja vya huku mikoani, kwa sababu pale anapofanya mazoezi na wenzake kuna kitu atakuwa anagundua nini anatakiwa afanye akiwa kwenye viwanja hivyo.

 

“Kubwa zaidi nilimuagiza achunguze kwa umakini mazingira ya viwanja hivyo kwa kutumia uzoefu wake, kwani akipata kitu huenda ikawa na faida kwangu kama mwalimu pamoja na timu kwa jumla kwa sababu bado tuna mechi nyingi ambazo tutacheza ugenini,” amesema Kaze.


Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 37 baada ya kucheza mechi 15 ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.

SOMA NA HII  NADO ATUPIA KAMBANI AZAM IKIITWANGA KMC 1-0 UWANJA WA UHURU