Home Uncategorized WAZAWA WAIPOTEZEA NAFASI YA SVEN BONGO,UONGOZI WASHANGAA

WAZAWA WAIPOTEZEA NAFASI YA SVEN BONGO,UONGOZI WASHANGAA


 BARBARA Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Simba amesema kuwa anashangazwa na makocha wazawa kushindwa kutuma CV zao kuomba kazi kubeba mikoba ya Sven Vandenbroeck.

Vandenbroeck ambaye alikuwa ni Kocha Mkuu ndani ya kikosi cha Simba alibwaga manyanga Januari 7 ikiwa ni muda mfupi kutoka aipeleke timu hiyo hatua ya makundi.

Ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum uliipa nafasi Simba kutinga hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya ushindi wa mabao 4-1 kwa kuwa mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe, Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Mtunguaji aliyempa tabu kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula kwa sasa atavaa jezi za rangi nyekundu na nyeupe baada ya kusaini dili la miaka miwili.

Gonzalez amesema kuwa kwa sasa mchakato wa kumsaka mrithi wa Vandenbroeck unaendelea baada ya kupokea jumla ya maombi ya kazi kutoka kwa mataifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ulaya isipokuwa mtu kutoka Tanzania.

“Wengi wameomba kazi ndani ya Simba kufundisha timu hii ambayo ni kubwa na inafanya vizuri ila nimeshangaa kuona kwamba hakuna kocha mzawa ambaye ameomba kazi.

“Kazi hii ni ya wote wenye uwezo hata wazawa pia wanapaswa wajitokeze ila hakuna ambaye ameomba kazi hii ni mbaya na inapaswa ifanyiwe kazi kwa makocha wazawa kuamini kwamba wanaweza kufundisha timu hizi zenye mashabiki wengi,” .

SOMA NA HII  SIMBA HAWANA DOGO, WALIANZISHA TENA KISA MTINDO WA UTAMBULISHO WA YANGA