BEKI SIMBA ATISHWA NA PACHA YA SAIDO, FISTON YANGA

 


BEKI wa zamani wa klabu ya Simba, Boniface Pawasa amesema kuwa ujio wa Fiston Abdoul Razak ndani ya kikosi cha Yanga utaiongezea timu hiyo makali kutokana na uwepo wa nyota, Saidi Ntibazonkiza 'Saido' ambao wataunda safu kali ya ushambuliaji.

Saido na Fiston wote wamesajiliwa katika kipindi cha dirisha dogo, ambapo wanaungana na kocha wao raia wa Burundi Cedric Kaze ambaye mpaka sasa hajapoteza mchezo wowote akiiongoza Yanga kwenye michezo 13.

Akizungumzia pacha hiyo Pawasa amesema: "Naona kabisa kutakuwa na pacha moja nzuri ndani ya kikosi cha Yanga kutokana na ujio wa Fiston kwa kuwa tayari yupo Saido.

"Tayari kila mmoja ameuona uwezo wa Saido tena ndani ya mechi chache tu, ambapo ameweza kufunga mabao na kuasisti hivyo kama ataungana na Fiston nadhani pacha yao inaweza kuwatesa wengi,"

Post a Comment

0 Comments