IBENGE:KWELI SIMBA WANAHITAJI HUDUMA YANGU


 FROLENT Ibenge, Kocha Mkuu wa Klabu ya AS Vita ya Congo pamoja na timu ya Taifa ya DR Congo amesema kuwa anatambua kwamba mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wanamhitaji.

Kocha huyo ambaye jana Januari 12 alikiongoza kikosi cha timu ya Taifa ya Congo kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars anatajwa kuwa kwenye hesabu za kuibukia ndani ya Simba.

Simba kwa sasa ipo visiwani Zanzibar ikiwa chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola ambaye amepewa mikoba ya Sven Vandenbroeck aliyechimba Januari 7 baada ya kile alichoeleza kuwa ni kuwa na matatizo ya kifamilia.

Kwa sasa Sven amepewa dili la miaka miwili kuinoa timu ya F.A.R ya Morocco jambo linalowafanya Simba waingie sokoni kusaka mbadala wake.

Ibenge amesema:"Simba ni timu kubwa na yenye ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika,hilo siwezi kukataa.

"Ninajua kwamba wanahitaji huduma yangu hilo lipo wazi hata msimu uliopita walinihitaji lakini shida ni kuwa kwa sasa mimi ni mwalimu wa AS Vita na Congo.

"Kama ningekuwa sina timu basi ningesema itakuaje lakini kwa sasa tusubiri na tuone bado nipo Congo na timu yangu ya AS Vita," amesema.

Post a Comment

0 Comments