Home Azam FC KOCHA AZAM AIPIGA HESABU ZA KUIMALIZA SIMBA

KOCHA AZAM AIPIGA HESABU ZA KUIMALIZA SIMBA


KOCHA mkuu wa kalbu ya Azam, George Lwandamina ameongeza msisitizo wa program za mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Simba. 

Huu utakuwa mchezo wa kwanza kwa Simba na Azam kukutana msimu huu ambapo unatarajiwa kupigwa Februari 4, mwaka huu ukiwa mchezo wa kwanza wa kiporo cha mzunguko wa kwanza wa ligi.

Kumbukumbu ya mwisho ya timu hizo kukutana ni ushindi wa mabao 3-2 walioupata Simba Machi 4, 2020 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili msimu uliopita.

Akizungumzia maandalizi ya ujumla kuelekea michezo yao ya ligi kuu, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ alisema: “Kikosi chetu kinaendelea na mazoezi kujiandaa na michezo ya mzunguko wa pili wa ligi, tulianza baada ya kukamilika kwa michuano ya Mapinduzi ambapo tilicheza michezo mitatu ya kujipima nguvu.

“Kati ya michezo hiyo tulishinda michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja, na kumalizia na mchezo dhidi ya KMC utakaopigwa leo.

“Michezo hii ni sehemu ya maagizo ya kocha Lwandamina ambaye kwa kutambua ugumu wa mchezo wetu wa kwanza wa ligi dhidi ya Simba utakaopigwa Januari 4, ameomba kupatiwa michezo mingi ya kujipima nguvu ili kukifanya kikosi chake kiwe tayari kwa mchezo huo dhidi ya Simba.

“Tunajua Simba wana kikosi kizuri na wameongeza nguvu kupitia usajili lakini hata sisi tumesajili na tumejipanga vizuri,”

SOMA NA HII  OBREY CHIRWA AWAACHIA VIONGOZI HATMA YAKE NDANI YA AZAM FC