KOCHA SIMBA: LOKOSA BADO SANA


 KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa mshambuliaji wake mpya, Junior Lokosa bado sana kuingia kwenye mfumo kwa kuwa hajawa fiti asilimia 100.

Lokosa amesaini dili jipya ndani ya Simba akitokea nchini Nigeria aliwahi kucheza ndani ya Esperance na alisaini dili la miezi sita Januari 25.

Tayari ameshaanza mazoezi na timu yake mpya ambayo leo itacheza mchezo wa ufunguzi kwenye mashindano mapya ya Simba Super Cup Uwanja wa Mkapa itakuwa ni dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Kocha huyo raia wa Ufaransa amesema:"Lokosa nimemuona ila bado hajawa fiti asilimia mia kwa sababu alikaa muda mrefu bila kucheza hii inatokana na janga la virusi vya Corona ambavyo vilifanya mambo mengi kusimama.

"Imani yangu ni kwamba kadri muda unavyozidi kwenda atakuwa bora na imara hivyo anahitaji muda ili kuimarika haitakuwa kwa haraka ambayo tunahitaji.

"Kuhusu mashindano ambayo tunashiriki ninasema kwamba ni mazuri na tutafanya vizuri hasa kwa kuwa wachezaji wamekuwa wakionekana wakifanya vizuri kwenye mazoezi," .

Post a Comment

0 Comments