YANGA KUWAFICHUA WABAYA WAO HIVI KARIBUNI

 MSHAURI Mkuu wa Klabu ya Yanga, Senzo Mbatha kuelekea mabadiliko amesema kuwa wanazidi kupambana ili kufikia malengo na wanatambua kwamba kazi ni kubwa kufikia malengo.

Mbatha alikuwa ndani ya Simba ambapo alikuwa Mtendaji Mkuu kabla ya kubwaga manyanga na kuibukia ndani ya Yanga.

Tayari umefanikiwa kutwaa taji la Mapinduzi ambalo ni la kwanza kwake akiwa na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze. 

Mbatha amesema:"Tuna kazi kubwa ya kufanya kwa sasa ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea kwa kuwa mipango mikubwa na lazima yatimie.

"Hatulali kwa kuwa wapinzani wetu pia hawalali hivi karibuni tutawafichua ili mashabiki waweze kuwajua," 


Post a Comment

0 Comments