BARBARA: UWEKEZAJI WA KWELI UNALETA MAFANIKIO KWENYE SOKA


 MTENDAJI Mkuu wa Simba, mwanadada Barbara Gonzalez amefunguka kuwa jambo pekee ambalo linaweza kuleta mafanikio kwenye soka ni uwekezaji wa kweli.

 

Barbara alieleza kuwa mpira wa sasa unahitaji uwekeze fedha ya kutosha kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo kwenye kununua wachezaji na kufanya maandalizi ya kina kwenye kila mchezo na mashindano makubwa kwa madogo.

 

Akizungumza kwa namna ambavyo Simba wanatisha msimu huu hasa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Barbara alifunguka: -Ukiwekeza kwenye soka unafanikiwa kirahisi kabisa bila hata wasiwasi. Hakuna ujanjaujanja kwenye soka.


“Ili uweze kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa lazima uwe na kikosi chenye wachezaji bora na kocha mwenye viwango vikubwa, ndicho ambacho sisi tunafanya, tumewekeza fedha kwa wachezaji na tunapata mafanikio.”


Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, ikiwa ipo hatua ya makundi, Simba inaongoza ligi ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 6.


Imecheza mechi mbili na kufunga jumla ya mabao mawili ilikuwa mbele ya AS Vita 0-1 Simba na Simba 1-0 Al Ahly.


Kesho inamchezo dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Mkapa mchezo wa ligi mzunguko wa pili.Post a Comment

0 Comments