BEKI HUYU MATATA WA KIMATAIFA AINGIA ANGA ZA SIMBA

 BAADA ya beki wa kulia wa timu ya AS Vita Club ya DR Congo, Shabani Djuma kuwasumbua Simba katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya mabingwa Afrika uliofanyika DR Congo, hatimaye uongozi wa Klabu ya Simba umeanza mazungumzo na mchezaji huyo kwa ajili ya kuhitaji huduma yake.


Beki huyo wa kulia ni mmoja wa manahodha wa kikosi cha AS Vita ambapo licha ya kuwa ni beki wa kulia lakini ndiye kinara katika utupiaji wa mabao katika kikosi cha AS Vita katika Ligi Kuu ya Congo mara baada ya kufunga mabao matano katika ligi hiyo msimu huu huku akiwapita baadhi ya washambuliaji wa timu hiyo.
Mmoja kati ya wachezaji wa kikosi cha AS Vita ambaye ni rafiki mkubwa wa beki huyo ambapo wote walicheza katika mchezo dhidi ya Simba, amesema kuwa ameambiwa na mchezaji huyo viongozi wa Simba wameanza kuulizia uwezekanao wa kumsajili mchezaji huyo mwisho wa msimu huu.

 

“Djuma ni rafiki yangu, tumekuwa wote AS Vita kwa muda sasa na wote ni manahodha katika kikosi hiki, ameniambia kuna viongozi wa Simba wanamfuatilia kwa ajili ya uwezekano wa kusajiliwa mwishoni mwa msimu huu, sijajua yeye kwa upande wake ataamua nini na anafikiria nini kuhusu Simba,” alisema kiungo huyo.

 

Simba licha ya kumuhitaji beki huyo ambaye anacheza upande wa beki wa kulia, katika nafasi hiyo wapo Shomari Kapombe na David Kameta ‘Duchu’.


Lemgo kubwa ni kuongeza nguvu kwa upande wa beki ili kuongeza nguvu sehemu ya ulinzi kuwa imara zaidi hasa kwenye mechi za kimataifa ambazo ushindani wake ni mkubwa.

Post a Comment

0 Comments