Home Azam FC DUBE AIPELEKA AZAM FC MIKONONI MWA POLISI

DUBE AIPELEKA AZAM FC MIKONONI MWA POLISI

 

PRINCE Dube, mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Azam FC amefanikiwa kutimiza majukumu yake kwa uzuri na kuipeleka timu hiyo hatua ya 16 bora Kombe la Shirikisho. 

Bao lake la ushindi dakika ya 45+1, Uwanja wa Azam Complex limetosha kuwafungashia virago Mbuni FC ambao walikamilisha dakika 90 bila kuweka mzani sawa.

Ushindi huo unaifanya Azam FC kuungana na Kagera Sugar, Simba,Yanga ambazo zimetinga hatua ya 16 bora.

Mchezo wake wa raundi ya tano watakutana na Polisi Tanzania,  Uwanja wa Azam Complex.

SOMA NA HII  NYOTA WAWILI WA AZAM FC KAZINI NA TIMU YAO YA TAIFA YA UGANDA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here