Home Yanga SC ISHU YA MKATABA WA CARLINHOS YANGA IKO HIVI

ISHU YA MKATABA WA CARLINHOS YANGA IKO HIVI

 


KUFUATIA kiungo wa Yanga, Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ kuwa nje kwa muda mrefu huku zikienea tetesi kuwa huenda mchezaji akaachwa mwishoni wa msimu huu, hatimaye zimemuibua Mjumbe wa kamati ya usajili wa Yanga na Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said ambaye amefunguka kuwa kiungo huyo bado yupo sana Yanga.

Raia huyo wa Angola alijiunga na Yanga katika usajili wa dirisha kubwa ambapo tangia ajiunge na klabu hiyo amekuwa akipatwa na majeraha ya mara kwa mara.

Akizungumzia kuhusu mkataba wa Carlinhos Injinia Hersi Said amesema kuwa mchezaji huyo wakati anasajiliwa na Yanga alisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu, hivyo wanatarajia kumuona akiendelea kucheza ndani ya timu hiyo mpaka mwisho wa mkataba wake na hawana mpango wa kumuacha mchezaji huyo.

“Carlinhos wakati anatua Yanga alisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu wa kuitumikia Yanga,hivyo ndiyo kwanza ametumika nusu mwaka, kabakiza mwaka mzima wa kuendelea kucheza na tunatarajia kumuona akiendelea kuichezea Yanga na si kumuacha kama inavyoelezwa.

“Kibaya kwake ni majeraha ambayo amekuwa akiyapata, lakini ni moja kati ya wachezaji wazuri ambao tumejaliwa kuwa nao ndani ya timu yetu, sisi kama viongozi tunaamini kuwa mzunguko wa pili atafanya mambo makubwa na ndio maana bado tunamuamini kuwa atatusaidia,”

SOMA NA HII  INJINIA HERSI USO KWA USO NA MANGUNGU....WADAU WAPISHA WAKAE WENYEWE...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here