KAGERE : HAO AL AHLY WAKIPANUA...NAINGIZA TENA..!!!


ZIMEBAKI saa zisizozidi 48 kabla ya Simba kushuka uwanjani kuvaana na Al Ahly ya Misri katika mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini straika nyota wa timu hiyo Meddie Kagere amefungua kinywa chake na kusema ‘Mwarabu lazima afe tena Kwa Mkapa’.

Kagere ndiye aliyefunga bao pekee lililoizamisha Al Ahly katika mechi yao michuano hiyo msimu wa 2018-2019 uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, enzi hizo ukijulikana kama Taifa siku ya Februari 12, 2019. Kagere alifunga dakika ya 65 na kulipa kiasi cha mabao 5-0 iliyiofungwa Simba ugenini jijini Cairo.

Akizungumza na Gazeti la Mwanaspoti, Kagere alisema ana uhakika alichokifanya siku ile kitajirudia tena kutokana na maandalizi wanayoyafanya kwa sasa kwa ajili ya mchezo huo wa Kundi A.

“Kama nitapata nafasi ya kucheza katika mechi hiyo ya Jumanne na tukatengeneza nafasi hata kama zikiwa chache kama ilivyokuwa mara ya mwisho naweza nikawapa furaha mashabiki wetu kwa kufunga bao tena. Tunataka kushinda tena tukiwa nyumbani,” alisema Kagere mwenye mabao tisa.

“Unajua tunakwenda kucheza na timu bora hapa Afrika iliyokamilika katika maeneo yote kwa maana hiyo tutakwenda kukutana na ushindani wa kutosha kutoka kwao ambao utachangia kutengeneza nafasi chache za kufunga na kama nitakutana na moja kati ya hiyo nitahakikisha naitumia,” alisema.

“Tumeweza kushinda ugenini ikiwa ni mwanzo mzuri kwetu kwani miongoni mwa malengo ambayo tulikuwa nayo huko walau tusiondoke bila ya pointi moja lakini tumefanikiwa kupata tatu. Tukifanikiwa kucheza vizuri na kuwafunga Al Ahly ni wazi tutamaliza vyema kundini.”

Kagere alisema kumaliza kileleni mwa kundi kuna faida mbili ya kwanza katika hatua ya robo fainali unapangiwa na timu ambazo hazina ubora, lakini hata mechi ya kwanza katika hatua hiyo utaanzia ugenini na kumalizia nyumbani,” alisema.


Post a Comment

0 Comments