KOCHA WA SIMBA SVEN KURUDI BONGO


 KAMPUNI ya Afrisoccer kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Kampuni ya La Liga kutoka Hispania, imeandaa kongamano la soka huku aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck akiwa mmoja wa watoa mada.

Kongamano hilo limepangwa kufanyika kati ya Machi 18 na 19, mwaka huu litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Maktaba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mratibu wa Kongamano hilo, Peter Simon, amesema kuwa wadau mbalimbali watashiriki mkutano wenye malengo ya kukuza na kuendelesha soka hapa nchini.

 

Simon aliwataja walengwa wa Kongamano hilo ni wadau wa soka ambao ni Serikali, Kamati za Michezo za Mikoa na Wilaya, TFF, Bodi ya Ligi Kuu Bara, klabu, Makocha na Mawakala wa Wachezaji.


Aidha aliwataja baadhi ya watoa mada katika Kongamano hilo ni Mlamu Mng’ambi (Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba), Senzo Mazingisa (Mshauri wa Yanga), Injinia Hersi Saidi (Makamu Mwenyekiti wa Usajili na Mashindano wa Yanga) na Martin Hamells (Wakala kutoka Ujerumani).

 

“Jumla mada sita zitakazowasilishwa katika Kongamano hili ambazo ni Masoko na Udhamini, Maendeleo ya soka la Vijana na Wanawake, Usimamizi wa Viwanja, Huduma za Uwakala, Vyanzo vya Mapato na Masuala ya Fedha kwa Klabu na Maendeleo ya Tehama na Soka.

 

“Tunaamini baada ya Kongamano hili baadhi ya klabu zitakuwa zimejifunza baadhi ya vitu na hasa jinsi ya uendeleshaji wa klabu, kwani lengo ni kuhakikisha soka linapiga hatua hapa nchini,” amesema Simon.Post a Comment

0 Comments