Home Yanga SC NYOTA MPYA YANGA FISTON ATAJA SABABU ZA KUTODUMU NDANI YA TIMU

NYOTA MPYA YANGA FISTON ATAJA SABABU ZA KUTODUMU NDANI YA TIMU


MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze, Fiston Abdul Razack amesema kuwa huwa hadumu kwa muda ndani ya timu nyingi kutokana na kupewa ofa kila wakati.


Ingizo hilo jipya kutoka nchini Burundi rekodi zinaonyesha kuwa amekuwa akikaa na timu kwa muda mfupi jambo ambalo linatoa picha kwamba atasepa pia ndani ya Yanga.

Miongoni mwa timu ambazo amcheza mwamba huyo ni pamoja na 1 de Agosto msimu wa 2017. Al Zawraa msimu wa 2018, JS Kabylie msimu wa 2018-19 na ENPPI msimu wa 2019-20.

Amesaini dili la miezi sita lenye kipengele cha kuongeza mkataba ndani ya timu hiyo inayoongoza ligi ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18.

Fiston amesema:”Nimekuwa nikipata ofa nyingi kila nikiwa kwenye timu jambo ambalo linanifanya nisiweze kudumu mahali ambapo huwa ninakuwa.
“Kikubwa ni kuona kwamba timu inapata mafanikio na kila mmoja analijua hilo, nipo sehemu sahihi na kila mchezaji anafurahia uwepo wangu ni imani yangu kwamba tutafikia malengo ambayo tumejiwekea,” amesema.

Anaungana na kiungo mshambuliaji Said Ntibanzokiza ambaye ni raia wa Burundi kama yeye.


SOMA NA HII  AZAM NA SIMBA MAJI YA SHINGO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here