PICHA YA SENZO MBATHA AKIWA NA KOCHA WA AL AHLY YAZUA GUMZO


USIKU wa kuamkia leo picha ya aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba,(CEO), Senzo Mbatha akiwa na Kocha Mkuu wa Al Ahly ya Misri imezua gumzo kwa mashabiki wa Simba na Yanga ambao wamekuwa wakibishana kuhusu picha hiyo.

Miongoni mwa mashabiki wa Simba ambao walianzisha mdahalo kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na Agnes Daniel ambaye ni maarufu kwa jina la Miss Simba.

Miss Simba ameenda mbali kwa kusema kuwa ilipaswa Senzo ambaye kwa sasa yupo zake ndani ya Yanga akiwa ni Mshauri Mkuu kuelekea kwenye masuala ya mabadiliko alipaswa asubiri mpaka mechi ikiisha aonane na watu wa Al Ahly.

Kcezoo Machalan ambaye ni shabiki wa Yanga amesema kuwa ni muhimu Watanzania kuwa na subira kwa kuwa mtu kufahamiana na mtu sio uadui.

"Yaani Bongo mwana yaaani mtu akijuana na mtu basi ana majukumu, hayo mambo yaachwe kwa familia ya michezo,".

Leo Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Al Ahly kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi, Uwanja wa Mkapa.


Post a Comment

0 Comments