SIMBA YAPEWA MBINU KUIMALIZA AL AHLY, WACHEZAJI WAONYWA


 FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Biashara United, amesema kikosi cha Simba kina uwezo wa kupata matokeo chanya mbele ya Al Ahly ikiwa watacheza kwa nidhamu na utulivu mkubwa.

 Leo Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Al Ahly ya Misri.


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 10:00 jioni na mashabiki 30,000 watapata fursa ya kushuhudia ndani ya Uwanja wa Mkapa ikiwa ni kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika,(Caf) kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona.Baraza amesema:-“Simba wameanza vizuri na wanaweza kupata matokeo chanya kwenye mechi za kimataifa, ila lazima waongeze nidhamu ndani ya uwanja na kupunguza makosa yasiyo ya lazima hasa kwa mabeki pamoja na viungo.

 

“Ikiwa watakuwa wanaruhusu makosa iwe ndani ya 18 ama karibu na 18 ni hatari kwao kwa kuwa wapinzani wao wanaweza kutumia kila nafasi na kugeuza kuwa bao, hapo umakini unahitaji,” alisema Baraza ambaye aliweka wazi kuwa wachezaji wa Simba wana tabia ya kupoteza muda.


Mchezo wa kwanza Simba ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya AS Vita ugenini inakutana na Al Ahly ambayo imetoka kushinda mabao 3-0 dhidi ya Al Merrikh hivyo Al Ahly wanaongoza kundi A wakiwa na pointi tatu sawa na Simba wakitofautiana kwa idadi ya mabao.


Bao la ushindi kwa Simba lilifungwa na Chris Mugalu kwa mkwaju wa penalti baada ya Luis Miquissone kumnawisha mchezaji wa AS Vita ndani ya 18.Post a Comment

0 Comments