Home Simba SC SIMBA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA WAARABU

SIMBA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA WAARABU


 MOHAMED Hussein, nahodha msaidizi wa Simba amesema kuwa morali ya wachezaji ni kubwa na wanaamini watapata matokeo chanya mbele ya Al Ahly ya Misri.

Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes inatarajiwa kusaka pointi tatu mbele ya Al Ahly, Februari 23, Uwanja wa Mkapa.

Tayari Waarabu hao wa Misri wameshawasili Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo na mashabiki 30,000 wataruhusiwa kuingia pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Hussein amesema:”Morali ya wachezaji ni kubwa na kila mmoja anahitaji ushindi hivyo tutapambana kupata matokeo mazuri mbele ya Al Ahly.

“Kila mmoja wetu anajua kwamba ushindani ni mkubwa, tunahitaji kufanya vizuri kwenye mechi zetu za kitaifa na kimataifa hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti,”.

Kwenye kundi A, Al Ahly anaongoza kwa idadi ya mabao mengi ambayo ni matatu anafuatiwa na Simba mwenye bao moja baada ya kuwafunga AS Vita DR Congo.

Wote kibindoni wana pointi tatu hivyo mshindi wa mchezo huo atajijengea ufalme nafasi ya kwanza.


SOMA NA HII  ISHU YA MANZOKI NA SIMBA SC....IMEBAKI HIVII TUU YANI....JAMBO LINAENDA KIMYA KIMYA....