WAARABU WATAJIWA DAU LA LUIS MIQUISSONE,NNE ZAWANIA SAINI YAKE


NYOTA wa Simba, Luis Miquissone mbali na TP Mazembe pamoja na Al Ahly kutajwa kuwania saini yake pia inaelezwa kuwa CD Belouizdad ya Algeria,Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini, Al Hilal ya Sudan.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ameweka wazi kwamba dau la mchezaji huyo sio la kitoto hivyo timu ambayo inahitaji kupata saini yake lazima ijipange.

"Uajua wengi wanauliza kuhusu Luis, yule ni aina ya wachezaji wa kipekee na wana uwezo mkubwa ndani ya uwanja hilo lipo wazi.

"Sasa tunajua kwamba kupitia mashindano haya ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa anachokifanya yeye pamoja na wachezaji wengine mawakala wanahitaji huduma yake sasa kumpata lazima zijipange kwa kweli.

"Naweka wazi kabisa dau la kumpata Luis kwa sasa ofa yake ya mwisho haiwezi kuwa chini ya Euro milioni moja hiyo ni ofa ya mwisho kabisa kwa mchezaji wetu.

"Dunia ya sasa inatumia Euro zaidi hivyo ofa yake haiwezi kuwa chini ya hiyo, nasema hivi hicho ni kiwango cha chini, kama Bwalya (Walter) kauzwa kwa dola milioni moja Al Ahly kwa nini Luis auzwe kwa chini ya kiwango hicho?

Nyota huyo amekuwa akitajwa kuwaniwa na timu nyingi kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja.

Mbele ya Al Ahly wakati Simba ikishinda bao 1-0 Uwanja wa Mkapa alitupia bao bora ambalo limezidi kumfanya awe gumzo.Post a Comment

1 Comments

  1. Price tag without concrete evidence who wants to buy him. If you want to get more than, the answer is simple... This player is NOT for SALE. That will make other teams to scratch their heads how they ├žan lure him out of your club. That's how to do business not telling them he's worth this or that. Shush it and leave it to the manager

    ReplyDelete