BOSSI SIMBA AFUNGUKA A-Z NAMNA WANAVYOSINDA MECHI ZAO 'KIMAFYA'


Simba imetoboa siri ya kupata mafanikio katika Ligi ya Mabingwa Afrika wakisema hayakuletwa kwa usiku mmoja kama baadhi wanavyodhani.

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Simba Salim  Abdallah 'Try Again amesema uongozi wao ukianzia bodi ya klabu hiyo imekuwa ikiishi katika ndoto za mafanikio ambayo wanayapata msimu huu.

Abdallah amesema baada ya kuweka mipango waliweka nguvu na umakini kuhakikisha wanafanikiwa kufika mbali na sasa ndoto yao inakaribia kutimia taratibu.

"Wapo wanadhani ni kama tumebahatisha kufikia hapa au tuliwaza ndani ya usiku mmoja na ikawa hapana,tulikuwa na malengo tukaweka nguvu ya kuhakikisha tunapambana ili tufanikiwe,"amesema Abdallah.

Bosi huyo amesema hata uundwaji wa kikosi chao umekuwa ukipitia hatua muhimu za maboresho kulingana na kila mapungufu wanayoyaona katika kila msimu.

"Kwa msimu wa nne sasa kama watu wanafuatilia vizuri tumekuwa tukiboresha kikosi chetu kwa umakini,hatukuwa tunasajili kwa papara kama ambavyo wengine wanafanya kila mchezaji aliyekuwa anakuja hapa ni kwa malengo na anastahili kuwa hapa."

Aidha Abdallah amesema katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo wako katika hatua ya makundi wanataka kufika mbali zaidi ya hatua ya robo fainali ambayo wakati wowote wakishinda mechi yao ijayo dhidi ya AS Vita watafuzu.

"Tumebakiza pointi moja kufika hatua ya robo fainali lakini Simba hatuwazi hapo tunataka angalau nusu fainali au hata fainali kama itawezekana."


Post a Comment

0 Comments