Home Simba SC JOASH ONYANGO KUSEPA BONGO, HALI YAKE IPO HIVI

JOASH ONYANGO KUSEPA BONGO, HALI YAKE IPO HIVI

 


BEKI kisiki wa Klabu ya Simba, Joash Onyango amesema kuwa yupo vizuri baada ya kupata maumivu Kwenye mchezo wao dhidi ya Al Merrikh. 


Jana Machi 16 wakati ubao ukisoma Simba 3-0 Al Merrikh,  Onyango alipata maumivu dakika ya 43 na nafasi yake ikichukuliwa na Erasto Nyoni. 


Hali yake ilionekana kuwatisha mashabiki kwa kuwa alitolewa akiwa amebebwa Kwenye machela.


Onyango amesema:”Nipo salama na ninaendelea vizuri natarajia kuelekea Kenya kwa timu ya Taifa,” 

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA MO DEWJI KULIA HASARA NA SIMBA....MCHAMBUZI MWINGINE AMZODOA JUMLA JUMLA...