Home Yanga SC WACHEZAJI WANAOSAJILIWA YANGA HAWANA HADHI YA KUCHEZA KIKOSI HICHO

WACHEZAJI WANAOSAJILIWA YANGA HAWANA HADHI YA KUCHEZA KIKOSI HICHO

 


MCHAMBUZI wa masuala ya michezo Tanzania, Mwalimu Alex Kashasha amesema kuwa tatizo kubwa linaloitesa Klabu ya Yanga kwa wachezaji wake kushindwa kufanya vizuri ni makosa ya ufuatiliaji wa wachezaji.


Kashasha amesema kuwa ikiwa watu watafuatilia kwa umakini aina ya wachezaji ambao wanaletwa ndani ya kikosi hicho kwa mbwembwe, wengi hawana hadhi ya kucheza ndani ya kikosi hicho jambo ambalo linafanya wawe na mwendo wa kusuasua.

Kutokana na mwendo wa kusuasua kwenye mzunguko wa pili chini ya Cedric Kaze raia wa Burundi pamoja na mzawa Nizar Khalfan ambaye alikuwa ni msaidizi walifutwa kazi Machi 7, uongozi wa Yanga uliamua kufuta benchi hilo la ufundi.

Alex Kashasha amesema:-” Makosa ambayo yanaigharimu Klabu ya Yanga ni moja yule  anayefanya scouting ndani ya Yanga anafanya ujanjaujanja mwingi kwa kuleta wachezaji ambao hawana hadhi ya kucheza ndani ya Yanga.

“Kwa mfano mchezaji kama Yikpe (Gnamien), aliwahi kuja Yanga na ubora wake haukuwa mkubwa akaondoka pia hakuwa na sifa za kucheza katika kikosi hicho.

“Mwingine ni David Molinga naye alikuja kwa mapambio mengi na hakuweza kufanya vizuri mwisho wa siku naye pia akaondoka.

“Kwa sasa kuna Saido Ntibanzokiza huyu ana unafuu ila ni majeruhi hapo unaona bado tatizo pia hata umri unaonekana kwamba umekwenda.

“Yacouba, (Sogne) huyu naye pia ni mgonjwa hivyo unaona kwamba bado kuna kazi kubwa ndani ya scouting ya Yanga.

“Mshambuliaji mwingine ni Michael Sarpong bado amekuwa anakimbiakimbia tu na zaidi ya mechi 21 ambazo amecheza ana mabao manne.

“Hivyo ni muhimu kwa Yanga kuweza kuangalia namna bora ya kufanya scouting ili kupata wachezaji ambao watakuwa na hadhi ya kucheza kwenye timu hiyo ikiwa wanahitaji mafanikio,” amesema.

SOMA NA HII  YANGA WATIKISA MBUYU NIGERIA....WAKIVUKA TU KUKUTANA NA VIGOGO HAWA NUSU FAINAL CAF...