Home Azam FC ZAYD KUREJEA NA DUBE

ZAYD KUREJEA NA DUBE


UONGOZI wa benchi la ufundi la klabu ya Azam umezidi kupata matumaini baada ya taarifa za kitabibu kutoka kwa madaktari wa timu hiyo, kuweka wazi kwamba nyota wawili wenye majeraha, Yahya Zayd na Prince Dube wanatarajia kurejea uwanjani mwanzoni mwa wiki ijayo.

Nyota hao ndiyo majeruhi pekee ambao wamebakia ndani ya kikosi cha Azam. Zayd alipata majeraha ya bega katika mchezo dhidi ya Mbeya City na kutakiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita.

Huku Dube yeye akiwa anasumbulkiwa na majeraha ya misuli ya paja, aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Mwadui na kutakiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili.

Akizungumzia hali za nyota hao, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Tumepata taarifa ya kitabibu kutoka kwa madaktari wetu kuhusu majeruhi wetu wawili ambao ni Dube na Zayd.

“Habari njema ni kuwa nyota hao wanaendelea vizuri na wanatarajiwa kuanza mazoezi mepesi mwanzoni mwa wiki ijayo, na tunatarajia pale timu itakaporejea watakuwa tayari kujiunga na wenzao kwa ajili ya maandalizi ya michezo yetu ijayo ya ligi,”

SOMA NA HII  AZAM WATAJA SABABU ZA KUPOKEA KICHAPO MBELE YA COASTAL UNION