Home Simba SC BAADA YA MECHI , KOCHA AL AHLY AMTAJA AISHI MANULA

BAADA YA MECHI , KOCHA AL AHLY AMTAJA AISHI MANULA


Wakati kocha wa Al Ahly, Pitso Mosimane akikiri timu yake kupata wakati mgumu mbele ya Simba jana nyumbani licha ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 amemtaja kipa Aishi Manula kwamba alikuwa kikwazo kwao kupata ushindi mnono katika mechi hiyo.

Mosimane alisema pamoja na kiwango bora kilichoonyeshwa na Simba katika mchezo huo uliochezwa jana usiku katika Uwanja wa Al-Salam, Cairo, juhudi binafsi za Manula pia zilichangia kufunga bao hilo pekee.

“Tuna furaha kwa kupata ushindi huu dhidi ya Simba.Tulikuwa na mechi nzuri dhidi ya mpinzani imara na tungeweza kupata mabao zaidi lakini kipa wao (Manula) aliokoa hatari nyingi ambazo zingeweza kuwa mabao,” alisema Mosimane.

Katika mchezo huo, Manula hasa katika kipindi cha kwanza alifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi mengi ya hatari ya Al Ahly ambayo yaliyoelekeza na Mohamed Afsha na Mohamed Sherrif ambayo yangeweza kuwafanya wapinzani wao wapate idadi kubwa ya mabao.

Manula amekuwa katika kiwango bora siku za hivi karibuni ambacho kimemfanya aokoe mashambulizi mengi ya hatari ya timu pinzani ambayo yangeweza kuwa mabao.

Na hilo limeifanya Simba kuwa na safu imara ya ulinzi ambayo imeruhusu mabao matatu tu katika mechi 10 za Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA WAKIWA NA REKODI KUBWA AFRIKA...SIMBA QUEENS NAO WASAKA KUWEKA HESHIMA CAF...