MORRISON KUWAKOSA WAARABU WA MISRI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

 


NYOTA wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, Bernard Morrison anatarajiwa kuukosa mchezo dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Aprili 9 nchini Misri.

Simba inatarajiwa kukwea pipa leo kuwafuata Waarabu hao wa Misri ambao ni wapinzani wao katika mchezo wa hatua ya makundi ukiwa ni mchezo wao wa mwisho huku wakiwa tayari wamekata tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali.

Kwenye kundi A, Simba inaongoza kundi ikiwa na pointi 13 huku Al Ahly ikiwa nafasi ya pili na pointi zake 8, zote zimetinga hatua ya robo fainali.

Morrison mwenye pasi mbili kwenye ligi ya mabingwa ataukosa mchezo huo kwa sababu ana kadi mbili za njano, moja alipata kwenye mchezo dhidi ya Al Merrikh na ya pili alipata kwenye mchezo dhidi ya AS Vita.

Kadi zote mbili Morrison alizipata Uwanja wa Mkapa na ile ya AS Vita alionekana akizinguana na mchezaji wa kikosi cha AS Vita ambaye alimchezea faulo jambo lililofanya mwamuzi wa kati pamoja na wachezaji kumtuliza Morrison ambaye alionekana kuwa damu imechemka.Post a Comment

0 Comments