EMANUEL OKWI NJIANI KURUDI SIMBA


 INAELEZWA kuwa nyota wa zamani wa kikosi cha Simba, Emanuel Okwi yupo kwenye hesabu za kurejea ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Dider Gomes.

Wakati kikosi cha Simba kilipotua nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly, aliwatembelea kambiniAprili 9 na kuzungumza na wachezaji wa Simba.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Al Salaam Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na kuwafanya waache pointi tatu mazima nchini Cairo ikiwa ni mchezo wao wa kwanza kupoteza hatua ya makundi baada ya kucheza mechi tano bila kufungwa.

Kwa sasa Okwi anacheza nchini Misri soka la kulipwa katika Klabu ya Ittihad ambapo msimu huu 2020/21 amecheza mechi 9 na kutumia dakika 493 na ametupia mabao mawili.

Alijiunga na timu hiyo msimu wa 2019/20 baada ya mkataba wake na Simba kuisha na kulikuwa na mvutano mkubwa kwenye upande wa kuongeza mkataba wake.

Ndani ya timu yake ya sasa nchini Misri mkataba wake unaisha msimu huu jambo ambalo linaongeza nafasi ya Simba kumtwaa mchezaji huyo bure.

Kuhusu suala hilo Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema:"Usiniulize kama Okwi ambae kwa sasa anacheza soka la kulipwa Misri atarejea kucheza Simba au laa msimu ujao ila jua kwamba mkataba wake na timu yake upo ukingoni,".Post a Comment

0 Comments