Home Namungo FC EXCLUSIVE: NAMUNGO YATAJA KUNDI LAO KUWA KIKWAZO

EXCLUSIVE: NAMUNGO YATAJA KUNDI LAO KUWA KIKWAZO


 UONGOZI wa Klabu ya Namungo FC umesema kuwa hayakuwa malengo yao kushindwa kutinga hatua ya makundi ila kundi ambalo walipangiwa lilikuwa na timu zenye ushindani mkubwa.

Ofisa Habari wa Namungo FC, Kidamba Namlia ameweka wazi kwamba walikuwa wanahitaji kupata matokeo ila kundi lilikuwa na timu ambazo zinaweza kutinga mpaka hatua ya fainali.

“Hapana baada ya kutinga hatua ya makundi hatukuwa na mpango wa kwenda kucheza tu ilimradi, ila wakati mwingine inabidi tuseme ukweli kwamba Namungo ilikuwa kwenye kundi gumu.

“Ilikuwa na Nkana, ilikuwa na Raja Casabalanca, Pyramids sasa hapo fanya kitu cha wazi kwamba uingie kwenye google search, andika Raja Casablanca.

“Maana yake sisi tulikuwa na washindani wawili ambao wawili Pyramids na Raja, hawa ni watu ambao sio wa kuishia hatua ya makundi wana nafasi ya kutinga hatua ya fainali kabisa, sisi tunakwenda kucheza nao kwenye hatua ya Kombe la Shirikisho, kutokana na ubora wao.

“Baada ya kufungwa bao 1-0 mchezo wa kwanza na Pyramids ugenini wao walizozana kwa kushinda bao hilo moja, sasa hapo unaona kwamba wao wamechukizwa na sisi kutufunga bao moja nasi tunachukia kwa nini tumefungwa.

“Kilichofuata Nkana alichukua tatu, Pyramids kachukua tatu, uwanja huohuo, hatufurahii ila tunajifunza,” amesema.

Kwenye kundi D, Namungo ikiwa inawakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho haijakusanya pointi baada ya kufungwa mechi zake tano na inashika nafasi ya nne.

SOMA NA HII  KOMBE LA SHIRIKISHO: NAMUNGO 0-3 RAJA CASABLANCA