KOCHA SIMBA AVURUGWA NA KADI ZA WACHEZAJI
 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa amekuwa akipata wakati mgumu pale wachezaji wake wanapoonyeshwa kadi za njano wakiwa kwenye kutimiza majukumu yake.

Raia huyo wa Ufaransa amekiongoza kikosi hicho kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika kikiwa na pointi 13 huku Al Ahly ikiwa na pointi 11 nafasi ya pili.

Akizungumza na Spoti Xtra, Gomes alisema kuwa imekuwa kazi kwake kupanga kikosi hasa pale wachezaji wake wanapokuwa na kadi za njano kwa kuwa zinavuruga mipango.

“Unajua kwenye mchezo hasa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ushindani ni mkubwa pale kadi inapotolewa kwa mchezaji ni lazima ufikirie namna ya kumlinda kwenye mchezo huo ama mchezo mwingine.

“Kila mchezaji ni muhimu kwenye kikosi jambo ambalo linafanya niwe ninaongea na wachezaji kwamba wanatakiwa kuwa makini, kwa kufanya hivyo kutapunguza yale makosa yasiyo ya lazima ila huwezi kuzuia yote,” alisema.

Miongoni mwa wachezaji ambao kwa sasa wana kadi za njano kwenye hatua ya makundi ni pamoja Joash Onyango, Shomari Kapombe, Thadeo Lwanga, Erasto Nyoni.Post a Comment

0 Comments