Home Azam FC LWANDAMINA: TUNAITAKA NAFASI YA YANGA

LWANDAMINA: TUNAITAKA NAFASI YA YANGA

 


BAADA ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kuwashusha Simba kutoka kwenye nafasi ya pili ya msimamo, kocha mkuu wa kikosi cha Azam, George Lwandamina amesema kuwa bado haridhishwi na nafasi waliyopo, na watapambana kusaka nafasi ya kwanza inayokamatiwa na Yanga.

Yanga ndiyo vinara wa msimamo wa Ligi na pointi zao 50 walizokusanya kwenye michezo 23, wakifuatiwa na Azam ambayo imefanikiwa kukusanya pointi 47 katika michezo 25 waliyocheza mpaka sasa.

Azam juzi walifanikiwa kuishusha Simba kutoka kwenye nafasi ya pili baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa, mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar.

Akizungumzia mipango yao, Lwandamina amesema: “Nafurahia kwa matokeo ya ushindi wa mabao 2-0 tulioupata dhidi ya Mtibwa Sugar, kama timu tunajua wazi kuwa matokeo yetu hayajawa ya kuridhisha sana msimu huu.

“Tumepata muda wa kurekebisha mapungufu tuliyokuwa nayo, na sasa tutahakikisha tunafanya vizuri zaidi ili kuweza kupanda juu zaidi kwenye msimamo, hatubweteki kwa na nafasi ya pili tuliyonayopo kwa kuwa tuna imani kuwa tunaweza kukwea juu zaidi kwenye msimamo,”

SOMA NA HII  AWESU AWESU NYOTA ANAYEPAMBANA NA HALI YAKE NDANI YA AZAM FC