MABOSI WA DORTMUND WAWEKA UGUMU USAJILI WA HAALAD
KLABU ya Borussia Dortmund imeweka wazi kuwa haina mpango wa kumuuza mshambuliaji wao Erling Haalad.

Nyota huyo amekuwa akitajwa kuingia kwenye rada za timu mbalimbali Ulaya ikiwa ni pamoja na Manchester United, Liverpool, Chelsea ambazo zinashiriki Ligi Kuu England hata Barcelona inayoshiriki La Liga imekuwa ikitajwa pia.

Mabosi wa Dortmund wameamua kumpigia simu wakala wa mchezaji huyo, Mino Raiola kwa nia ya kumjulisha kwamba hawana mpango wa kumuuza nyota huyo.

Mabosi wa Dortmund wameweka wazi kuwa wanaweza kubadili maamuzi hayo ikiwa hawatafuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya na inaelezwa kuwa tayari Raiola ameanza mazungumzo na timu zinazohitaji huduma yake ikiwa ni pamoja na Barcelona.

Nyota huyo alisajiliwa ndani ya kikosi hicho akitokea Klabu ya Red Bull Salzburg, Januari 2020.Post a Comment

0 Comments