MANULA AINGIA ANGA ZA MAMELODI SUNDOWNS
KIPA namba moja wa Simba, Aishi Manula inaelezwa kuwa amewekwa kwenye anga za timu kubwa za Afrika Kusini pamoja na Sudan ambazo zinahitaji kupata saini yake.

Manula amekuwa kwenye ubora ndani ya uwanja baada ya kuwa sehemu ya kikosi cha Simba ambacho kimetinga hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwenye mechi sita za hatua ya makundi alikaa langoni kwenye mechi tano huku lango lake likiwa salama kwenye mechi tatu ilikuwa AS Vita 0-1 Simba, Simba 1-0 Al Ahly na Simba 3-0 Al Merrikh. Alitunguliwa mechi mbili ilikuwa Simba 4-1 AS Vita na Al Ahly 1-0 Simba.

Mechi moja dhidi ya Al Merrikh ugenini alikaa langoni kipa namba mbili Beno Kakolanya naye aliyeyusha dakika 90 bila kufungwa.

Kutokana na uwezo wa Manula habari zinaeleza kuwa Al Merrikh ya Sudan pamoja na Mamelodi Sundowns nao wanahitaji saini yake.

Kuhusu hilo Manula amesema kuwa kwake ni furaha kuhitajika na timu mbalimbali ila bado ana mkataba na mabosi wake Simba.Post a Comment

0 Comments