MKATA UMEME WA SIMBA LWANGA AKANA KUCHEZA RAFU


 TADDEO Lwanga,  kiungo wa timu ya Simba meibuka na kubainisha wazi kwamba yeye hachezi rafu kama wengi wanavyosema badala yake anakuwa anatimiza majukumu yake.

 Mkata umeme huyo ameongeza kwamba kwa nafasi yake kama kiungo mkabaji inabidi ajitume kwa ajili ya kulilinda lango lake ambapo kama angekuwa anacheza rafu angekuwa anatoka mchezoni.

 

Lwanga mara nyingi amekuwa akicheza soka la kutimiza majukumu yake ya kuhakikisha lango lao halipati kushambuliwa na wapinzani wao kwenye mechi zao za ligi kuu au Ligi ya Mabingwa Afrika.


Raia huyo wa Uganda huyo amesema kuwa: “Hapana, hapana, mimi sichezi rafu, ila kama kiungo mkabaji natakiwa kuwa makini mchezoni muda wote. Kama ningekuwa nacheza hivyo ningekuwa natoka sana mchezoni, lakini sifanyi hivyo hata kidogo.

 

“Naisaidia timu kushinda mechi zake na hilo ndiyo jambo ambalo nalifanya mara zote, natimiza majukumu yangu kwa kulilinda vyema lango la timu yangu," .


Lwanga ni miongoni mwa wachezaji wa Simba waliopo nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi unaotarajiwa kuchezwa kesho, Aprili 9.


Timu zote mbili tayari zimetinga hatua ya robo fainali kwenye kundi A ambapo Simba inaongoza kundi ikiwa na pointi 13 na Al Ahly ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 8.Post a Comment

0 Comments