MSHAMBULIAJI MRUNDI FISTON KUONDOKA MAZIMA YANGA


 MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Abdulazack kwa sasa muda wake wa kuishi Bongo upo ukingoni baada ya mkataba wake wa miezi sita kuwa kwenye hatua za mwisho kukamilika.

Raia huyo wa Burundi alisaini dili la miezi sita na pale msimu utakapokwisha naye inaelezwa kuwa atapewa mkono wa kwa heri.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa nyota huyo zimeeleza kuwa tayari ameshaambiwa kwamba hataongezewa mkataba kwa kuwa bado hajaonyesha yale makali ambayo alikuwa nayo.

"Fiston kwa sasa muda wake umeisha na anajua kwamba hataongezewa mkataba kwani kazi ambayo alikuwa amepewa inaonekana bado haijaeleweka," ilieleza taarifa hiyo.

Raia huyo wa Burundi ndani ya ligi amefunga bao moja ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania wakati wakigawana pointi mojamoja na ana bao moja kwenye Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora ilikuwa dhidi ya Ken Gold.

Hivi karibuni Fiston alisema kuwa anatambua uwezo wake na alisaini dili la miezi sita kwa kuwa hajawahi kudumu na timu kwa muda mrefu kutokana na ofa ambazo huwa anapata.

"Sijawahi kuwa kwenye timu moja kwa muda mrefu kwa sababu huwa ninakuwa na ofa nyingi sina tatizo na uwezo wangu,".Post a Comment

0 Comments