Home Simba SC SABABU YA MIRAJI ATHUMAN KUACHWA SIMBA YAWEKWA WAZI

SABABU YA MIRAJI ATHUMAN KUACHWA SIMBA YAWEKWA WAZI


IMEFAHAMIKA wazi kuwa kumbe Kocha Mkuu wa Simba, raia wa Ufaransa Didier Gomes Da Rosa alilazimika kumuengua kwenye kikosi kilichosafiri kwenda Misri, Miraji Athuman ‘Sheva’, kwa sababu  alimuachia programu za mazoezi afanye na Perfect Chikwende raia wa Zimbabwe.

 Simba ilipokwea pipa kwenda nchini Misri kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji wao Al Ahly,kwenye msafara Gomes alimuweka kando Sheva.

 Mchezo huo uliochezwa Aprili 9, ubao ulisoma Al Ahly 1-0 Simba na kuwafanya Waarabu hao wa Misri kulipa kisasi cha kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 walipocheza na Simba, Uwanja wa Mkapa mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi.

Habari zimeeleza kuwa Sheva aliachwa makusudi na Gomes ili aweze kufanya mazoezi ya pamoja na Chikwende kwani ana mpango mkakati wa kuwatumia katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara.

Tayari kikosi cha Simba ambacho kinaongoza kundi A na kimetinga hatua ya robo fainali kikiwa na pointi 13 kimesharejea Bongo kwa ajili ya maandalizi ya mechi za ligi.

Mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO