SIMBA SC WASHUSHA BASI JIPYA LA KISASA..KUANZA KUTUMIKA KESHO..!!


KLABU ya Simba imeamua kufanya kweli baada ya kuwashushia wachezaji wake gari lingine aina ya TATA Marcopolo (New Model) kwa ajili ya shughuli za safari ya klabu hiyo katika Ligi za ndani.

Inaelezwa kwamba gari hilo liliingia nchini mapema mwaka huu na mwezi huu limeanza kuwekwa stika rasmi za klabu hiyo kwa ajili ya kuanza matumizi.

Awal Simba walikuwa wanatumia gari aina ya Yutong lililotengenezwa mwaka 2012 na kudumu nalo mpaka leo hii.

Gari hilo jipya Tata Marcopolo linamuonekano maridadi na tayari limeanza kubandikwa stika mchana wa leo zenye nembo za wadhamini wa klabu hiyo.

Wakati gari hilo likiwa katika hatua za mwisho kukamilika, Uongozi wa klabu ya Simba tayari umetangaza kuliuza gari yao ya zamani aina ya Yutong.

Post a Comment

0 Comments