Home Simba SC SIMBA YAPANIA KUSHINDA MECHI ZOTE ZA LIGI KUU BARA

SIMBA YAPANIA KUSHINDA MECHI ZOTE ZA LIGI KUU BARA


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa mpango wake kwenye mechi za Ligi Kuu Bara ni kuona anashinda zote ambazo zimebaki ili kutimiza lengo la kutwaa ubingwa wa ligi.


Kwenye msimamo wa ligi, Simba ambao ni mabingwa watetezi wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 46 baada ya kucheza mechi 20, vinara ni Yanga wenye pointi 51 baada ya kucheza mechi 24.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Gomes alisema kuwa anatambua changamoto ambazo zipo kwenye ligi hilo halimpi tabu hesabu zake ni kuona wachezaji wake wanashinda mechi zao.

“Tunahitaji kutimiza mipango ambayo ipo baada ya lengo la kwanza la kutiga hatua ya robo fainali kutimia kwa kuwa tunarudi kwenye ligi ili turudi lazima tufanye maandalizi. Tunahitaji kushinda mechi zote ambazo tutacheza.

“Sababu ya kufanya hivyo ni kuona malengo ya Simba yanatimia kwani tunahitaji kutwaa ubingwa wa ligi na ili uwe bingwa lazima ushinde mechi zako.

“Kuna mechi tutacheza nyumbani na nyingine tutacheza ugenini hivyo tunajiandaa kwa ajili ya mechi zote ambazo tutacheza na tupo tayari,” alisema.

Aprili 14, Simba itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Mtibwa Sugar iliyotoka kuambulia kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo wa kwanza walipokutana na Simba, Uwanja wa Jamhuri Morogoro, ubao ulisoma Mtibwa Sugar 1-1 Simba.

SOMA NA HII  SIMBA WAJIBU HOJA ZA DK KIGWANGALA...TRY AGAIN AMSHUKIA JUMLA JUMLA...AMPELEKA BUNGENI KWA 'SHANGAZI'....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here