SIMBA YAVUJISHA SIRI ZA MFARANSA GOMES

 


PASCAL Wawa, beki kisiki wa kikosi cha Simba amesema kuwa siri kubwa ambayo wanayo katika mapambano ya kuzuia hatari za wapinzani wao ni maneno ya Kocha Mkuu, Didier Gomes, raia wa Ufaransa kuwataka wasikubali kufungwa.

Katika Ligi Kuu Bara, safu ya ulinzi ya Simba inashika namba moja kwa kuruhusu mabao machache ikiwa ni mabao 10.

Safu ya ulinzi ya Mwadui inashika namba moja kwa kufungwa mabao mengi ambayo ni 53 baada ya kucheza mechi 28.

 Wawa amesema kuwa kila mara wamekuwa wakisistizwa na Gomes wasikubali kuokota mpira kwenye nyavu zao hivyo wao wanafuata maelekezo na kutimiza majukumu yao.

“Safu yetu ya ulinzi ina wachezaji wenye kujiamini na wanatimiza majukumu kwa umakini. Ukianza na mimi pia, Onyango, (Joash) Kenedy, (Juma), hata Nyoni, (Erasto). Maagizo ambayo tumepewa na mwalimu, (Gomes) tusikubali kufungwa.

“Imekuwa hivyo kwenye mechi zetu zote zile za Ligi ya Mabingwa Afrika hata Kombe la Shirikisho tumekuwa tukifanya kazi yetu, hivyo furaha yetu ni kuona kwamba hatufungwi,” amesema Wawa.

Kwenye msimamo wa ligi Simba inaongoza ikiwa na pointi 61 baada ya kucheza jumla ya mechi 25.     

Post a Comment

0 Comments