SIMBA YAWEKA WAZI SABABU YA KUWATEMA NYOTA WAKE WA KIGENI WAWILI MAZIMA

 


BAADA ya kutoonekana kwenye michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wachezaji wa Simba waliosajiliwa kwa ajili ya michuano hiyo, Junior Lokosa raia wa Nigeria na Mzimbabwe Peter Muduha, klabu hiyo imefunguka kuwa sababu ya kuachana nao ni Kocha Mkuu, Didier Gomes kutofurahishwa na viwango vyao.

Lokosa ambaye yeye ni mshambuliaji alisajiliwa na Simba akitokea Esperance ya Tunisia huku beki kisiki, Peter Muduha akitokea Highlanders FC ya Zimbabwe.

Wachezaji hao walisajiliwa Januari, mwaka huu kwa ajili ya michuano ya kimataifa ambapo mpaka sasa Simba imefuzu kuingia hatua ya robo fainali huku wachezaji hao wakiwa hawajacheza mchezo wowote.

“Wachezaji waliosajiliwa hivi karibuni kwa ajili ya kucheza michezo ya kimataifa ambao ni Junior Lokosa na Peter Muduha watavunjiwa mikataba yao hivi karibuni.

“Wamekuwa na timu kwa muda mrefu lakini bado viwango vyao havikuwa bora vya kumridhisha Kocha Gomes, hivyo huenda wakasitishiwa mikataba yao mwishoni mwa msimu huu,” alisema mtoa taarifa huyo.

Aidha, kwa upande wa Gomes wakati Simba ikielekea Sudan kumenyana na Al Merrikh alisema: “Wachezaji niliowaacha ambao hawapo kwenye kikosi kinachosafiri akiwemo Peter Muduha na Lokosa Junior sijafurahishwa na viwango vyao.”

Post a Comment

0 Comments