WAWILI WA SIMBA KUIKOSA KARIAKOO DABI MAZIMA KWA MKAPA


 BEKI wa kati wa Simba Ibrahim Ame anatarajiwa kuukosa mchezo wa Kariakoo Dabi, kati ya Simba na Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 8, Uwanja wa Mkapa.

Beki huyo ambaye ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba akitokea Klabu ya Coastal Union ya Tanga amefungiwa na Kamati ya Masaa 72.

Hali hiyo inatokana na kufungiwa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara katika kikao cha Aprili 27,2021 baada ya kupitia matukio na mwendo wa Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili.

Ame amefungiwa mechi tatu na faini ya laki tano kwa kosa la kumzuia mwamuzi msaidizi kufanya maamuzi yake ilikuwa ni kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina FC.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Gwambina Complex, Aprili 24, ubao ulisoma Gwambina 0-1 Simba na bao la ushindi lilifungwa na Mohamed Hussein kwa shuti kali la guu la kushoto akiwa nje ya 18.

Mbali na Ame pia nyota Francis Kahata naye ataukosa mchezo huo kwa sababu yeye jina lake lipo kwenye orodha ya wachezaji watakaoshiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Post a Comment

0 Comments