Home Yanga SC BEKI YANGA ANASUBIRI RIPOTI YA MADAKTARI

BEKI YANGA ANASUBIRI RIPOTI YA MADAKTARI


 BEKI wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amefichua kuwa kwa sasa anaendelea kupata huduma ya matibabu kutokana na kusumbuliwa na tatizo la misuli, huku akisisitiza anasubiri kauli ya madaktari aweze kurejea uwanjani.

Ninja ametoa kauli hiyo baada ya kukosekana katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara ambapo pia ataukosa mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Mwadui unaotarajiwa kupigwa kesho Jumanne kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ninja amesema kwa sasa anaendelea na matibabu, lakini hajui lini atarejea uwanjani kwa kuwa tatizo lake lipo chini ya uangalizi wa daktari wa timu hiyo.

 

“Sijui siku gani nitarejea uwanjani, lakini jambo kubwa bado naendelea kupata matibabu kutokana na tatizo linalonisumbua, lakini namshukuru Mungu hadi sasa nipo sawa licha ya kwamba bado tiba haijaisha.

 

Nadhani nitaiwahi mechi ya Simba, lakini bado kila kitu kinahitaji maombi namna matibabu yanavyokwenda maana hata ukiangalia tupo kwenye ushindani mkubwa wa kupigania ubingwa wa ligi kuu kutokana na mechi ambazo zimebaki,” alisema Ninja.


Chanzo: Spoti Xtra

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUPIGWA JUZI....YANGA WALAMBA MKATABA NA UMOJA WA MATAIFA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here