Home CAF CAF YAONGEZA IDADI YA WACHEZAJI WA AKIBA

CAF YAONGEZA IDADI YA WACHEZAJI WA AKIBA


 SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF) limeongeza idadi ya wachezaji wa akiba kutoka 7 hadi 9 kuanzia hatua ya Robo Fainali itakayochezwa tarehe 14 Mei, 2021.

Aidha kuhusiana na idadi ya wachezaji watakaoingia kwenye mechi moja CAF wanasema vilabu vitataarifiwa hivi karibuni baada ya marekebisho yanayotarajiwa kufanywa na FIFA kupitia IFAB (International Football Association Board) ambao wanahusika na marekebisho ya sheria na kanuni.


Habari hiyo itakuwa njema kwa timu ambazo zinashiriki  Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kwa Tanzania, Simba wapo hatua hiyo wakiwa wananolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes. 

Pia Mashirikisho/Vyama vya Soka vimetaarifiwa kuviambia vilabu vitakavyoshiriki Mashindano yajayo ya CAF (Inter club Competitions) kwa msimu wa 2021/2022 kuwa wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kwa Kamati ya Mashindano ya CAF kupitia CMS (Competition Management System) sio zaidi ya tarehe 30 Juni, 2021.

Taarifa hiyo ilitolewa na Caf, Mei 3, 2021 kwa ajili ya nchi zote za Afrika ambazo zinashiriki mashindano ambayo yanaandaliwa na Caf.



SOMA NA HII  KOMBE LA SHIRIKISHO KUFUTWA... RAIS CAF "SIKUWEKA PESA MAKUSUDI...AMEFUNGUKA HAYA