COASTAL UNION HESABU ZAO NI LIGI KUU BARA


 JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa kwa sasa hesabu zake kubwa ni kwenye mechi za Ligi Kuu Bara baada ya kuondolewa kwenye hatua ya 16 bora, Kombe la Shirikisho.

Coastal Union iliondolewa na Mwadui FC hatua ya 16 bora kwa kufungwa mabao 2-0 na kuwaacha wapinzani wao wakitinga hatua ya robo fainali, Uwanja wa Mwadui Complex.

Mgunda amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zilizobaki ndani ya ligi ili waweze kusalia ndani ya Ligi Kuu Bara.

"Nguvu kubwa kwa sasa ni kwenye mechi zetu za ligi na tuna amini kwamba tutafanya vizuri kikubwa ni kuona kwamba tunabaki ndani ya ligi.

"Kila mchezaji anatambua kwamba ushindani ni mkubwa na kila timu ambayo tunakutana nayo inahitaji ushindi, tupo tayari na mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema.

Kwenye msimamo wa ligi, Coastal Union ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 33 baada ya kucheza mechi 28.Post a Comment

0 Comments