Home Yanga SC ISHU YA USAJILI YANGA WAMPA RUNGU NABI, WENGINE KUONGEZEWA MIKATABA

ISHU YA USAJILI YANGA WAMPA RUNGU NABI, WENGINE KUONGEZEWA MIKATABA


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi kuelekea msimu ujao ameachiwa rungu kuhusu ishu ya kuijenga Yanga ya ushindani zaidi.

 

Msimu huu Yanga imeonekana inasuasua kiasi cha timu hiyo kubadilisha benchi lake la ufundi mara tatu. Ilianza na Kocha Zlatko Krmpotic, kisha Cedric Kaze kabla ya ujio wa Nabi.

 

Kamati ya Usajili na Ufundi ya Yanga, imesema kwamba, inasubiri ripoti ya benchi la ufundi ambayo wanatarajia kukabidhiwa kabla ya kumalizika msimu huu wa 2020/21, kisha baada ya hapo kufanya usajili wa fasta ili kumkabidhi kocha majembe mapema aanze kuyanoa.


Akizungumza na Spoti Xtra, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga, Dominick Albinus, alisema: “Kwa sasa tunasubiri ripoti ya Kocha Mkuu na benchi lake la ufundi kuona mapendekezo yao kuelekea msimu ujao.

 

 

“Tutaanza kufanya vikao vya kupitia mapendekezo ya usajili baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo ambayo tunatarajia kuipokea kabla ya kumalizika kwa msimu huu.

 

“Tutahakikisha katika kipindi cha usajili tunatengeneza timu ambayo itakuwa na ushindani mkubwa ya kupigania makombe yote ambayo yatakuwa mbele yetu.


“Kwa msimu huu bado timu inaendelea kupambana mpaka mwisho wa ligi ili kujua ni kitu gani ambacho tunaweza kuvuna lakini lengo letu la ubingwa lipo palepale, halijabadilika.

 

“Kuelekea msimu ujao, tutawaongezea mikataba baadhi ya wachezaji na kufanya usajili mzuri kwa ajili ya kuleta ushindani, kisha tutamuachia kocha afanye kazi yake.” amesema.

SOMA NA HII  WINGA TELEZA WA TP MAZEMBE AKUBALI KUTUA YANGA...NI YULE ALIYEMTESHA ULIMI DJUMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here