PRINCE DUBE WA AZAM APEWA TUZO YA MEDDIE KAGERE

 


KOCHA Msaidizi wa kikosi cha Azam, Vivier Bahati, amefunguka kuwa ana imani kubwa kuwa mshambuliaji wao, Prince Dube anaweza kutamatisha utawala wa misimu miwili wa mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere kwa kutwaa tuzo ya ufungaji bora msimu huu.

 

Dube amekuwa na ushkaji mkubwa wa kucheka na nyavu ambapo kwenye mchezo wa Kombe la FA hatua ya 16 bora alifanikiwa kufunga mabao mawili mbele ya Polisi Tanzania.


 Mabao hayo yameipa nafasi Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina kutinga hatua ya robo fainali na kwenye ligi ametupia mabao 12 akiwa ni namba moja anafuatiwa na Meddie Kagere wa Simba mwenye mabao 11.

 

Kagere ndiye anakamatia tuzo hiyo ambayo ameitwaa kwa misimu miwili mfululizo ambapo katika msimu wa 2018/19 aliweka kambani mabao 23, huku msimu uliopita wa 2019/20 akifanikiwa kumaliza msimu na mabao 22.

 

Bahati  amesema: “Ni jambo lililo wazi kuwa Dube ni miongoni mwa washambuliaji bora kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kwa sasa.

 

“Japo kuna baadhi ya upungufu wa ufundi ambao tunaufanyia kazi, ambapo naamini baada ya kurekebisha hayo yatazidi kumfanya awe bora na kuna uwezekano mkubwa akaibuka mfungaji bora msimu huu.”Post a Comment

0 Comments