SIMBA: YANGA NI TIMU BORA, TUTAPAMBANA KUPATA POINTI TATU


 NAHODHA wa Simba, John Bocco, amefunguka kuwa wanakwenda kupata ushindi mnono mbele ya watani zao, Yanga, watakapokutana Mei 8, 2021 Uwanja wa Mkapa.

Bocco amesema anafahamu kuwa mchezo huo hautakuwa rahisi kwao lakini kwa namna ambavyo wanajiamini na kutaka alama tatu kwenye mchezo huo, haoni nafasi ya Yanga kuchomoka.


Nahodha huyo mzawa amesema anajua mchezo huo utakuwa mgumu kwa kuwa Yanga walianza msimu vizuri na hata sasa, bado wanacheza vizuri lakini wao wana wachezaji bora na watajipanga ili kuhakikisha wanatoka na ushindi kwenye mchezo huo.


“Mchezo utakuwa mgumu na wala siyo rahisi kama ambavyo watu wanafikiria, Yanga wanacheza vizuri tangu mwanzo wa msimu, lakini sisi tuna wachezaji bora na tutajipanga na kuondoka na alama tatu.


“Niwaombe mashabiki waendelee kutusapoti kwa kuwa tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo na tutapambana ili kufanya vizuri," .


Mchezo wa kwanza walipokutana Novemba 7, ubao ulisoma Yanga 1-1 Simba na kuwafanya wagawane pointi mojamoja. Post a Comment

0 Comments