UJANJA WA MUGALU WA SIMBA NI KWA MKAPA


 MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, ujanja wake wa kucheka na nyavu ni Uwanja wa Mkapa ila akitoka hapo imekuwa ngumu kwake kufurukuta.

Sababu kubwa imebainishwa na Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola ni ugumu wa viwanja vya nje ya Dar kuwapa ugumu wachezaji wao kucheza kwa uhuru jambo linalowakosesha ile ladha ambayo wameizoea.

Simba ikiwa imecheza mechi 25 ndani ya ligi na kutupia mabao 58, Mugalu ametupia mabao 8 na katika mabao hayo ni mabao mawili alitupia nje ya Dar, moja ilikuwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mbele ya Kagera Sugar na moja ilikuwa mbele ya JKT Tanzania, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Kwa Mkapa ametupia mabao sita jambo linaloonesha kwamba hapo ndipo ujanja wake ulipo. Aliwafunga Biashara United, Gwambina FC,  Ihefu, JKT Tanzania hawa aliwatungua bao mojamoja na mabao mawili aliwafunga Dodoma Jiji ilikuwa ni Uwanja wa Mkapa.

Matola ameliambia Spoti Xtra:”Ukiacha Uwanja wa Kaitaba nje ya Dar, viwanja vingine miondombinu yake ni migumu kuweza  kucheza mpira wa pasi na kupata matokeo inakuwa ngumu jambo linalofanya tushinde ila kwa tabu,” .Post a Comment

0 Comments