Ticker

6/recent/ticker-posts

DSTV BANNER

AZAM FC WAMUONGEZA MKATABA WA MIAKA MIWILI DUBE


KLABU ya Azam imemaliza utata na mshambuliaji wake matata, Prince Dube baada ya kumsainisha makataba wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Mkataba huo umesainiwa leo jioni mbele ya Ofisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Abdulkarim Amin 'Popat' baada ya kuelewana katika mazungumzo.

Usajili wa mchezaji huyo unamaliza kelele zote za awali zilizokuwa zinaendelea katika kuhusishwa na kujiunga katika klabu ya Simba.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi za mchezaji huyo kutajwa kwamba anaweza kujiunga na Simba lakini mabosi wa Azam walikanusha kwa kusema hatoweza kuondoka.

Gazeti la Mwanaspoti liliwahi kuzungumza na Popat kisha aliweka wazi sababu kubwa ya kutoweza kumuuza mchezaji huyo imetokana na wapo katika hatua za kujenga timu imara.

Dube mpaka sasa ndiye kinara wa ufungaji katika Ligi Kuu akiwa ameifungia timu hiyo mabao 14 huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Meddie Kagere na John Bocco wenye mabao 11.

Huu ni msimu wa kwanza kwa mchezaji huyo lakini amegeuka kuwa muhimili mkubwa katika safu ya ushambuliaji Azam baada ya kuonyesha ubora katika kufumania nyavu.

Reactions

Post a Comment

0 Comments