Home Yanga SC ISHU YA METACHA MNATA KUSAJILIWA SIMBA IPO HIVI

ISHU YA METACHA MNATA KUSAJILIWA SIMBA IPO HIVI


 WAKATI tetesi zikieleza kuwa kipa namba moja wa Yanga, Metacha Mmata anahitajika ndani ya Simba, kocha wa makipa Milton Nienov amesema hana mpango wa kuongeza kipa mpya.

Raia huyo wa Brazil amesema kuwa anakubali uwezo wa makipa alionao kwa sasa hivyo atafanya nao hao kazi.

Makipa hao ni Aishi Manula,  Beno Kakolanya na Ally Salim jambo linalomfanya asipate nafasi kufikiria usajili mpya.

Metacha amekuwa akihusishwa na Simba na ila kwa sasa alitajwa kuwa na utovu wa nidhamu jambo lililosababisba akaondolewa katika msafara uliokuwa Shinyanga na hakucheza mchezo wa robo fainali dhidi ya Mwadui katika Kombe la Shirikisho.

Kocha huyo amesema:”Kwa sasa hapana sina haja ya kipa mpya maana nina furaha na makipa nilionao,”. 

SOMA NA HII  YANGA WAMKUNJULIA ROHO FEI TOTO...JINA LAKE KUTAJWA KWENYE FAINAL YA CAF JUMAPILI...