NYOTA WAWILI WASEPA YANGA, WENGINE HAWA WANNE WANAFUATA


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa nyota wao wawili wameondoka tayari katika kikosi hicho kwa ajili ya kujiunga na timu zao za taifa.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa tayari wachezaji hao wameshakwenda nchini kwao huku wale ambao wameitwa timu ya taifa ya Tanzania, taifa Stars watakuwa kambini kwa muda mpaka muda wa kuripoti kambini utakapofika.

"Mukoko, (Tonombe) na Yacouba, (Songne) hawa tayari wamekwisha ondoka kwenye timu na kwenda kujiunga na timu zao za taifa.

"Wengine ambao wameitwa timu ya taifa hawa watakuwa kambini na wataondoka kuelekea kambini pale siku itakapowadia wakitokea kambini," amesema.

Wachezaji wa Yanga ambao wameitwa timu ya taifa ni pamoja na Metacha Mnata, Dickson Job, Lamine Moro na Feisal Salum.

Tonombe yeye ameitwa timu ya taifa ya Congo na Yacouba ameitwa timu ya taifa ya Burkina Faso.


Post a Comment

0 Comments