RUVU SHOOTING: YANGA WATATUSAMEHE, HAMNA NAMNA


 MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting ameweka wazi kuwa wapinzani wao Yanga inabidi wawasamehe kwa kuwa hawana chaguo la kufanya mbele yao zaidi ya kuwafunga.

Kikosi cha Ruvu Shooting kitaingia kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga kikiwa na kumbukizi ya kupoteza mchezo wao mbele ya watani wa jadi wa Yanga ambao ni Simba kwa kufungwa mabao 3-0 Uwanja wa CCM Kirumba.

Bwire amesema kuwa watajipanga kwa mechi yao ijayo dhidi ya Yanga ili kupata matokeo na wanaamini inawezekana kutokana na soka safi wanalopiga vijana wao.

“Wapinzani wetu Yanga watatusamehe kwa kweli mahali ambapo tupo na kitu ambacho tunahitaji ni pointi tatu kama ambazo wao wanahitaji ila wasifikiri kwamba itakuwa kazi rahisi, moto wa vijana wa Ruvu Shooting sio wa mchezo.

"Kupoteza kwetu mbele ya Simba haina maana kwamba hatupo bora wala imara hapana, ukweli ni kwamba tupo vizuri na tutawafuata wapinzani wetu kwa hesabu kali kupata pointi tatu," amesema.

Ruvu Shooting ipo nafasi ya 10 imekusanya pointi 37 baada ya kucheza mechi 30 inakutana na Yanga yenye pointi 61 nafasi ya pili itakuwa ni Juni 17. 


Ikiwa Ruvu Shooting ipo nafasi ya 10 na pointi 37 itakutana na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 61.Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Juni 17, saa 1:00 usiku.Post a Comment

0 Comments