WATATU SIMBA WATAJWA KUOMBA KUCHEZA AZAM FC


 IMEELEZWA kuwa nyota watatu wa Simba wamewekwa kando kwenye mpango wa kujiunga na Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina.

Nyota hao ni pamoja na kiungo Ibrahim Ajibu, beki Gadiel Michael pamoja na Francis Kahata raia wa Kenya ambao wanatajwa kuomba kucheza ndani ya timu hiyo.

Ajibu ambaye mkataba wake unameguka msimu huu ndani ya Simba habari zimeeleza kuwa moja ya wasimamizi wake aliongea na uongozi wa Azam FC ili kuweza kuona namna gani wataweza kumsajili ila mabosi hao walimtolea nje kwa kuweka wazi kwamba hakuna nafasi.

Pia Gadiel naye alikuwa anahusishwa kujiunga na timu hiyo jambo ambalo limekuwa gumu kukamilika.

Kuhusu Kahata pia habari zinaeleza kuwa alikuwa anatazamwa na Azam FC ili ajiunge nao na kwa sasa yupo huru jambo lolote linaweza kutokea.

Habari zinaeleza kuwa Kahata yupo huru kwa sasa kwa kuwa uongozi wa Simba umegoma kumuongezea mkataba wake.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit ameweka wazi kwamba hakuna nyota wa Yanga ama Simba ambao wameomba kujiunga na Azam FC.Post a Comment

0 Comments